Mfumo rasmi wa Kongoo ya Kiswahili
Maswali na Majibu Barua Pepe
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA

(BAKITA)
YA KISWAHILI

Kuhusu Kongoo

Kongoo ni hazina ya kidijitali ya Kiswahili inayosimamiwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).

Dhumuni la Kongoo

Kongoo inalenga kuwezesha utafutaji, uhifadhi na uchambuzi wa matini mbalimbali za Kiswahili kwa wanafunzi, watafiti, waandishi na jamii kwa ujumla.

Mchango kwa maendeleo ya Kiswahili

Mfumo huu unasaidia kuandaa, kuhifadhi na kufikisha hazina ya lugha ya Kiswahili kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Matini hupitiwa na kuidhinishwa kabla ya kuchapishwa.

Huduma kuu

  • Utafutaji wa maneno, vifungu vya maneno na matini.
  • Uchambuzi na uhusishaji wa matini kwa makundi.
  • Usajili wa waandishi na kumbukumbu za machapisho.
  • Ukaguzi na uidhinishaji wa matini kabla ya kuchapishwa.

Picha na nembo

Nembo ya Taifa na nembo ya BAKITA ni faili rasmi zilizotolewa kwa mradi. Picha za Mlima Kilimanjaro, wanyamapori wa Serengeti, Mwalimu Julius K. Nyerere (1975) na Abeid Amani Karume (1964) zimehifadhiwa ndani ya mfumo kutoka Wikimedia Commons. Leseni na chanzo vya kila picha lazima viheshimiwe kabla ya matumizi nje ya Kongoo.